29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

NIGERIA: WASICHANA 82 WAACHIWA HURU NA BOKO HARAM

 

 

Ofisi ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana katika mji wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mwaka 2014, wameachiwa huru.

Maofisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na kuamua kubadilishana wanafunzi hao na wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.

Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya bweni katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wasichana wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles