23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Nigeria wajiandaa kupiga kura leo

LAGOS, NIGERIA

KAMPENI za uchaguzi zimemalizika nchini Nigeria kwa rais anayemaliza muhula wake, Muhammadu Buhari, kusifu kipindi chake cha uongozi, huku mpinzani wake mkubwa, Atiku Abubakar, akiwatolea wito wafuasi wake wahakikishe wanamnyima kura na kung’oa kabisa utawala wa Buhari.

Atiku Abubacar amewatolea wito mkali wafuasi wake waliokusanyika katika jimbo alikozaliwa la Adamawa wahakikishe enzi za Buhari zinamalizika.

Hayo yamejiri siku moja baada ya wagombea kuahidi mbele ya wanadiplomasia, wasimamizi wa uchaguzi na wananchi, watahakikisha uchaguzi unafanyika salama.

Wagombea wote wawili, Atiku aliyewahi kuwa makamu wa rais na Buhari mtawala wa zamani wa kijeshi anayesema amegeuka kuwa mwanademokrasia, wanatokea kaskazini mwa Nigeria. Wapiga kura milioni 84 watateremka vituoni kesho kumchagua mmoja kati ya viongozi hao wawili.

Wakati huo huo,  wagombea wamesema wapo tayari kwa zoezi la uchaguzi mara baada ya kumalizika kampeni, ambapo wapiga kura milioni 84 wanatarajiwa kupiga kura.

Katika kambi inayomuunga mkono kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Atiku Abubakar Mjini Lagos wafuasi wake wamejitokeza kumuunga mkono.

Walifanya kampeni za mwisho wakiwa na imani kuwa, mgombea wao atashinda kama alivyoniambia mfuasi huyu:

“Tunamhitaji Atiku aje atuongoze sasa hivi, tumechoka kuteseka, tunawaomba sana Wanigeria wampigie kura Atiku, uchumi wetu utaimarika na mambo yatakuwa mazuri,” alisema mmoja wa wafuasi wake.

Kwa upande wa chama tawala cha APC, wao walitumia matarumbeta katika eneo la Ikoyi, katikati mwa mji huu, kumwombea Rais Buhari kura.

Mfuasi huyu anaamini kuwa Rais Buhari anastahili kurejea tena madarakani.

“Buhari anajenga msingi, msingi wa maendeleo, ukweli na kupinga ufisadi, sababu hizi ndizo zilizotufanya kuacha kazi zetu na kuja hapa kumuunga mkono ili Nigeria iendelee,” alisema Buhari.

Kuelekea uchaguzi wa kesho, Rais Buhari ambaye anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wake, Atiku Abukakar, alikuwa na ujumbe huu kwa raia wa Nigeria.

Atiku naye alituma ujumbe wake wa mwisho kabla ya siku ya upigaji kura. Wagombea 72 wanawania urais, lakini ushindani ni kati ya Rais Muhammadu Buhari na makamu wa rais wa zamani, Atiku Abubakar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles