Nigeria kuuza ndege mbili za Rais

0
616

ndege-nigeria

Katika kuhakikisha uchumi wa Nigeria unatengamaa, serikali ya nchi hiyo  imeamua kuuza ndege mbili kati ya 10 zinazotumiwa na Rais. Uamuzi huo umelenga  kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Uamuzi huo wa kuuza ndege hizo unakwenda sambamba na  kuzihamishia  ndege zilizobakia  kwa shirika la ndege la nchi hiyo kwa dhamira ya  kuongeza ufanisi ndani ya shirika hilo.

Nigeria ni moja kati ya nchi zenye uchumi mkubwa  Afrika. Hata hivyo  kwa kipindi kirefu sasa uchumi wake umekuwa ukiyumba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here