26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

NIDA ijitafakari ugawaji vitambulisho

SERIKALI imesema mwisho wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole ni Desemba 31, mwaka huu.

Uamuzi huo  umetangazwa juzi na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye bungeni mjini Dodoma akiwataka Watanzania kutimiza wajibu huo  wasizimiwe simu zao.

Usajili wa laini za simu unaanza Mei mosi mwaka huu, usajili mpya wa laini za simu utaanza na moja ya masharti yaliyowekwa  i upate usajili, ni kuwa na Kitambulisho cha Taifa.

Kwa kuwa kazi hii iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, tumeona ni vema tukatoa dukuduku letu   kuhakikisha Watanzania wengi wanatendewa haki.

Tangu kutolewa kwa tangazo hili yamekuwapo   maswali mengi kutoka kwa wananchi wa kawaida ambao wengi wao hawana vitambulisho vya taifa, jambo ambalo linaonekana wazi kuwa kikwazo kwao.

Kama tunavyotambua Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndiyo imepewa dhamana ya kuhakikisha kila mwananchi anapata kitambulisho chake, lakini ndani ya mamlaka hiyo kuna baadhi ya mambo yanakwenda ndivyo sivyo.

Tangu mamlaka ianze kazi ya kusambaza vitambulisho  mwaka 2012, mpaka sasa kuna mamilioni ya Watanzania hawajapata vitambulisho licha ya kutumia mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Tunasema hivyo kwa sababu  mamlaka   imekuwa na utaratibu mbovu mno wa usambazaji wa vitambulisho  kwa muda mrefu, jambo ambalo limezua malalamiko mengi kutoka kwa wananchi waliojiandikisha.

Kwa mfano, mamlaka  imekuwa na utaratibu wa kupeleka vitambulisho vilivyo tayari makao makuu ya wilaya kwa maofisa wake, kisha wao huwaita watendaji wa serikali za  mitaa  kuvipeleka maeneo husika.

Katika eneo hili ndiko kumejaa mwenendo mbovu ambao umesababisha vitambulisho vingi kushindwa kuwafikia walengwa kwa wakati.

Leo hii  baada ya viatmbulisho kufikishwa mitaani huko, hakuna matangazo yoyote  yanayotolewa na NIDA kwa wananchi waliojiandikisha kwenda kuchukua vitambulisho vyao, badala yake vinalundikana ndani ya ofisi za mitaa  na mwisho wa siku huharibika.

Tunasema haya kwa sababu ushahidi tunao, tumetembelea ofisi nyingi za serikali za mitaa katika Wilaya ya Ubungo,  Dar es Salaam na kukuta mamia ya vitambulisho vikiwa vimelundikwa bila wahusika kupewa taarifa.

Tunajiuliza hivi kwa nini Serikali inatumia gharama kubwa ya kuchapa vitambulisho halafu vinapokamilika havifikii walengwa kwa wakati? Nani anajibika katika  hali? Ndiyo kusema maofisa wa NIDA walioko kwenye wilaya zao huwa hawapati mrejesho wa ugawaji wa vitambulisho hivyo?

Pia inasikitisha kuona vitambulisho vya mtaa A vinapelekwa mtaa C na  hakuna ofisa wa mamlaka  anayelitambua hilo na kusababisha wananchi wengi kutaabika mno kutafuta na kukosa majibu ya msingi.

Tunayasema kwa nia njema kabisa  serikali ione tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi wa haraka kabla ya mambo hajaenda kombo zaidi.

Kama kweli kodi za Watanzania zinatumika hapa, basi ni vizuri  vitambulishi  vikawafikia walengwa kuliko kuendelea kuozea serikali za mitaa    

Tunatambua  haya hayako mijini tu, bali huko vijijini wananchi wengi wanalalamika mno kwa kukosa vitambulisho tangu wengi wao wajiandikishe.

Tunaisihi NIDA ijitafakari vizuri kwenye utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho hivi haraka   viwafikiwe wahusika.  Kama hawaamini hali hiyo ni wakati mzuri wa wao kutuma maofisa wake katika maeneo mbalimbali kwenye ofisi za serikali za mitaa   watafute njia mbadala  ya kugawa vitambulisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles