NICKI MINAJ, FUTURE WASITISHA ZIARA YAO

0
817

 

CALIFORNIA, MAREKANI


RAPA Nicki Minaj amethibitisha kusitisha ziara yake ya muziki, kutokana na mauzo madogo ya tiketi Kaskazini mwa Amerika.

Ziara hiyo ambayo inayojulikana kwa jina la NICKIHNDRXX Tour, alikuwa anashirikiana na rapa Future lakini mrembo huyo aliamua kuweka wazi mara baada ya kufanya shoo kwenye tamasha la tuzo za MTV Video Music Awards.

“Kutokana na mambo ambayo yamekuwa nje ya uwezo wetu, tumeamua kusitisha ziara yangu na Future, lakini bado mashabiki wataendelea kupata burudani kuanzia Mei 19 mwakani, hivyo ninaomba radhi mashabiki wangu kutokana na usumbufu uliojitokeza,” alisema Nicki.

Ziara hiyo ilipangwa kuwa sehemu ya msanii huyo kuitangaza albamu yake mpya ya ‘Queen’ ambayo ameiachia siku za hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here