20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

NICKI MINAJ ATHIBITISHA KUTOKA KIMAPENZI NA EMINEM

LOS ANGELES, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa Marekani, Nicki Minaji amethibitisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa mkongwe wa nchi hiyo, Marshall Bruce, maarufu Eminem.

Kauli hiyo iliyotolewa wikiendi hii na Minaj inakuja baada ya kuposti video katika ukurasa wake wa Instagram akiupa kiki wimbo wa ‘Big Bank’ ulioimbwa na 2 Chainz, Big Sean na YG.

Akiwa katika harakati hizo Minaj alikutana na swali kama yupo katika uhusiano na Eminem ambapo alijibu ‘ndio’.

Kutokana na jibu hilo Eminem pia aliposti katika ukurasa wake:“Mpenzi wangu unajua ukweli…..” na  dakika chache Minaj alijibu kwa kusema: “Mpenzi wangu nilijua tungefanya siri hadi siku ya harusi.”

Minaj alikuwa akihusishwa  kutoka kimapenzi na Nasir Jones maarufu kama Nas, baada ya kuachana na Meek Mill pamoja na Safaree Samwels.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles