22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Nicki Minaj afunga ndoa kimya kimya?

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, amewashtua mashabiki zake baada ya kubadilisha jina la kwenye akaunti yake ya Twitter na kujiita Mrs Petty.

Kitendo cha kubadili jina kumeacha maswali mengi kwa mashabiki huku wakiamini tayari rapa huyo amefunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake Kenneth Petty.

Wiki mbili zilizopita wawili hao walifanikiwa kupata kibali cha kufunga ndoa ambapo kibari hicho hudumu kwa siku 90 tangu kukipata, hivyo wiki iliopita Nicki aliweka wazi kuwa watafunga ndoa ndani ya siku za kibari hicho.

Mashabiki wanaamini tayari wawili hao wamefunga ndoa japokuwa kati yao hakuna aliyeweka wazi kama kweli wamefanikisha jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles