25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nichagueni nipaishe maendeleo- Ndalichako

Na Editha Karlo,Kasulu

MGOMBEA ubunge  Jimbo la Kasulu  Mjini, Profesa Joyce Ndalichako (CCM), amewataka wananchi wa Wilaya ya Kasulu  kumchagua kuwa mbunge wao ili aipaishe wilaya hiyo kwa maendeleo.

Amesema  atafanya kazi kubwa ya kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi sambamba na kusimamia masuala muhimu ya wananchi.

Ndalichako aliyasema hayo juzi kwenye viwanja vya Umoja mjini Kasulu wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za ubunge.

 Aliwaomba wananchi kukichagua chama chake  ili kiweze kushika dola. Alisema  tahakiksiha anaendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara ya ndani ili kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao.

“Mimi sikuwa mwanasiasa, nilipata ubunge wa kuteuliwa ila nina ifurahia, siasa ninaipenda, waomba wananchi wa Kasulu Mjini mnichague niwe mtumishi wenu niwaletee maendeleo,” alisema.

Alisema miaka mitano ijayo, ilani ya chama imeelekeza kuhakikisha wanapata tija katika mazao yao na vijiji vyote ambavyo havina umeme na maji vinapata huduma hiyo ili kufanikisha mpango wa Serikali ya CCM  hadi kufikia mwaka 2025, Tanzania inakuwa nchi ya kuigwa barani Afrika.

“Mimi ni mwanamke mpambanaji,mnyenyekevu naweza kwenda popote nikajishusha na kuomba nikasikilizwa mkinichagua nitakuwa kinara wa kupambania maendeleo, nitapambana hadi kieleweke”alisema

“Wakati nikiwa mbunge wa kuteuliwa nimefanya mengi katika wilaya yetu,sekta za miundombinu ya elimu,kutoa mikopo kwa kina mama na vijana na kuboresha miundombinu ya barabara za ndani nipeni miaka mitano niwe mtumishi wenu mnitume jambo lolote nitafanya.

“Sasa nawaomba wana Kasulu wenzangu tumpe kura nyingi za ushindi wa kishindo Rais wetu John  Magufuli na madiwani wote msinichanganyie rangi za madiwani, nawaombeni sana nipe madiwani wa chama cha mapinduzi ili jifanye nao kazi vizuri,”alisema

Mbunge mteule kundi la vijana (UVCCM), Sylivia Sigula aliwataka wananchi kuchagua mafiga matatu ambayo ni rais,mbunge na madiwani ili waweze kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wanaKasulu kwa kushirikiana.

“Nawaomba mumpe kura nyingi za kishindo Rais wetu John Magufuli pia mchague madiwani wote wa chama cha mapinduzi ili waweze kumsaidia mbunge kufanya kazi mkimchanganyia madiwani mtakuwa mmevunja miguu hataweza kutembea,pia ukinununua tochi mpya katika tochi hiyo ukaweka betri mbili na gunzi moja hiyo tochi itawaka kweli?mmenunua tochi iwekeni betri tatu ili iweze kuwaka vizuri”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles