28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

NIC yatoa msaada kwa wanawake wa CCBRT

Mwandishi wetu

Benki ya NIC imeadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wanaopatibiwa matibabu ya ugonjwa wa fistula katika Hospitali ya CCBRT.

Akizunguma wakati wa kutoa misaada hiyo Mkurugenzi wa benki hiyo, Magret Karume amesema benki yake ni moja kati ya taasisi zinazojali suala la usawa ikiwa ni pamoja na ajira na kuongeza kuwa benki hiyo inathamini jamii inayoizunguka na huzisadia katika nyanja ya elimu, afya na mazingira.

“Tunafurahi kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani pamoja wanawake hapa CCBRT, kusaidia jamii inayotuzunguka na wanawake ni moja kati ya vipaumbele vya benki yetu kwani unapomsaidia mwanamke unasaidia jamii nzima na nchi kwa ujumla.

“Ili kusaidia jamii inayotuzunguka tumeamua kutumia siku hii kuimarisha uhusiano wetu na hospitali ya CCBRT. Benki yetu leo imeamua kuja hapa na kutoa misaada mbali mbali itakayowasidia wanawake wanopata matibabu ya fistula hospitalini hapa,” amesema Margaret.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles