24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 13, 2024

Contact us: [email protected]

NIC yanadi bima ya kilimo Maonesho Nanenane

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Dodoma

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limewataka wakulima kulinda mazao yao kwa kuyakatia bima ya kilimo ili kujilinda dhidi ya majanga mbalimbali.

Shirika hilo linaanza kulinda kilimo kwenye shamba la kuanzia hekta 100 ambapo wakulima wadogo wanaweza kuungana katika vikundi au kupitia vyama vya msingi ili kupata hekta hizo ambazo zitapatiwa bima hiyo.

Akizungumza Agosti 3,2024 na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Karimu Meshack, amesema yanapotokea majanga wanamrudishia mkulima kile alichokuwa amekiwekeza katika kilimo.

NIC yanadi bima ya kilimo Maonesho Nanenane

“Tupo kwenye maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu na kuwashawishi wakulima waweze kulima salama kwa kuhakikisha wanakuwa na bima ya kilimo kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya nchi.

“Kama mkulima aliwekeza Sh milioni 500 endapo akipata majanga tunamrudishia ili alime tena, akiwa hajakata bima ile Sh milioni 500 inakuwa imepotea na itamgharimu kwenda kuzitafuta ili aende akalime,” amesema Meshack.

Amesema katika Mkoa wa Kilimanjaro baadhi ya wakulima wameshanufaika na bima hiyo ambapo NIC iliwalipa zaidi ya Sh milioni 255 ili waendelee kulima.

Mkurugenzi huyo amesema mwitikio wa wakulima kwenye bima hiyo ni mkubwa na kuwahamasisha wakulima wengine kuchangamkia fursa hiyo.

“Kwenye kilimo kuna mambo mengi mkulima anaweza akalima na kukutana na ukame, mvua nyingi zilizokithiri zikaharibu mazao au wadudu.

“NIC inataka mkulima alime na yale majanga
yanayoambatana na kilimo atuachie ili mtaji aliowekeza kwenye kilimo usipotee…tunamkinga mkulima na majanga yatakayotokea,” amesema.

Amesema pia wanatoa huduma za bima za maisha, mali na ajali na kuwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kujilinda dhidi ya majanga mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles