26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

NIC kuboresha Bima kwa viwango vya Kimataifa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Bima ya Taifa NIC) imeelza kuwa katika kusheherekea miaka 60 wataendelea kutoa huduma bora na za kidigitali kwani katika miaka yote wameweza kujua hitaji la wananchi na wamejipanga kutoa huduma bora na zenye tija.

Akizungumza Julai 5, jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk. Elirehema Doriye baada ya kutembelea banda hilo nan kusisitiza kwamba miaka 60 kwa NIC ni kuzaliwa upya kwani kumepelekea kukua na kufika viwango vya Kimataifa.

“Miaka 60 imetupa hekima ya kuelezea Watanzania na kujua wanataka nini na tunamuangalia mteja uwezo wake hivyo inatusaidia kumhudumia vizuri hali iliyotupelekea kwendana na viwango vya kimataifa kwa kiwango kisicho pungua asilimia 90,” amesema Dk. Doriye.

Aidha, Dk. Doliye amesema wanaendana na mabadiliko ya uchumi na teknolojia katika utoaji huduma kutokana bidhaa zinazopatikana kwenye bima hiyo na uhitaji wa soko.

Amesema bidhaa ambazo wanatengeneza kwenye bima hiyo ni pamoja na bima za kawaida, maisha na zinginezo ambapo huduma hizo zinapatikana kidigital hali inayochochea ukuaji wa uchumi.

Sambamba na hayo, Dk. Doriye amesema mafanikio waliyoyapata ni kutokana na maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuifungua nchi kiuchumi na kuruhusu uwekezaji unaofanywa nchini.

“Miaka 60 ya NIC sisi kwetu ni kuzaliwa upya katika kutoa huduma kwani historia inatusaidia kujua leo ili kuiandaa kesho,”ameongeza Doriye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles