28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

NI VITA YA SARRI, EMERY LEO

LONDON, ENGLAND


MAKOCHA wawili wapya, Maurizio Sarri wa Chelsea na Unai Emery wa Arsenal, leo kwa mara ya kwanza wanatarajia kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa Uwanja wa Stamford Bridge.

Klabu zote zimefanya mabadiliko katika dirisha la usajili lililopita, zikiwa na matumaini kwamba zinaweza kupata mafanikio.

Mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, Chelsea iliifunga Huddersfield mabao 3-0 wakati Arsenal ikianza kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Manchester City.

Mchezo huo unaonekana kutoa muda wa ziada kwa makocha hao kujenga vikosi vyao kabla ya kufurahia mafanikio.

Sarri atahitaji kushinda mchezo wa kwanza akiwa nyumbani wakati Emery hataitaji kupoteza tena baada ya kichapo cha mchezo uliopita.

Chelsea imeifunga Arsenal mara 62 lakini imepoteza mara 76. Timu hizo zimewahi kutoka sare mara 52, ikijumuisha mara mbili msimu uliopita.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Huddersfield, Eden Hazard, alitumika kama mchezaji wa akiba ila inawezekana Sarri akamwanzisha dhidi ya Arsenal.

Hata hivyo, inawezekana Hazard kuanza kikosi cha kwanza akichukua nafasi ya Willian da Silva au Pedro Rodriguez au akacheza nafasi ya ushambuliaji ambayo hucheza Alvaro Morata ambaye kwa sasa hayupo katika kiwango bora.

Arsenal wanahaha kufanya uchaguzi safu yao ya ulinzi, Unai Emery, anaumiza kichwa kupata chaguo sahihi kumtafuta beki wa kushoto.

Kuumia kwa Ainsley Maitland-Niles katika mchezo dhidi ya Manchester City, aliungana na Nacho Monreal na Sead Kolasinac, ambao wote wapo majeruhi.

Emery anaweza kumtumia Stephan Lichtsteiner ambaye aliziba pengo la Maitland-Niles, kocha huyo pia ataendelea kumtumia Petr Cech  dhidi ya  kipa mpya, Bernd Leno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,491FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles