22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ni kazi ngumu kuepuka vifo kwa mahujaji Saud Arabia

02DC54EA-FBAE-456F-8923-908F4A140991_mw640_mh360_sMWAKA 2014 tarehe kama hizi nilikuwapo Saudi Arabia kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya Hijja. Sikuwapo kwenye makundi yanayohudumiwa na mawakala wa mahujaji kutoka Tanzania, bali nilikwenda huko nikiwa mgeni wa serikali ya Mfalme wakati huo Marehemu Mfalme Abdullah bin Abdulaziz. Huyu wa sasa alikuwa msaidizi wake.

Niliungana na wanahabari kutoka vyombo vikubwa na vidogo kutoka barani Afrika, Asia na Ulaya. Mbali na kufanya ibada ya Hijja, serikali ya nchi hiyo ilituwezesha kutembelea maeneo mengi ya kihistoria ambayo ni vigumu kutembelewa na mahujaji na kufuatilia kila hatua ndani na nje ya Ibada ya Hijja.

Mojawapo ya zoezi tulilolifanya ni kuruka angani na helikopta za serikali kwa ajili ya kuangalia zoezi la ibada ya hijja. Tuliona na kukumbana na mambo mengi na hata tulipokutana na Waziri wa Habari na Utamaduni wan chi
hiyo, kwenye hafla ya kushukuru kumaliza kwa ibada hiyo ya mwaka 2014, tulishauri mambo tisa ya kurekebishwa.

Mojawapo ya mambo tuliyoishauri serikali ya nchi hiyo ni kuangalia upya shughuli za Tawaf (Kufu) kuzunguka
kaaba mara saba. Safari ya kutoka viwanja vya Arafat kwenda Muzdalifa na zoezi la utupaji mawe kwenye eneo la
Jamarati. Nina hakika serikali haikuufanyia kazi ushauri wetu na ndio maana kumetokea zahama ya vifo.

Inawezekana kutokea kwa vifo vya mahujaji mara mbili pale Msikiti Mkuu wa Makkah na kule kwenye eneo la Jamarati ambapo mahujaji hupaswa kutupa kokoto kwa idadi maalumu kwa siku tatu mfululizo, katika minara
mitatu iliyojengwa kwenye mstari mmoja unatokana na mabadiliko ya uongozi wa juu.

Kifo ni njia pekee ya kufika kwa Mola hivyo, si kitu cha kuogopa. Ufanyaji ibada ya Haj unaweza kuwa chanzo cha
kufika kwa Mwenyezi Mungu. Mara nilipopata habari za vifo vilivyotokea katika minara ya Jamarati, nilizungumza na mwanahabari mwenzangu Abdulaziz – Al- Rabi’ee wa Saudi Gazette, akanielezea mkasa wote ulivyokuwa.

Ibada ya Haj huanza Agosti toka mfungo tatu uandame, Mahujaji wote hutakiwa kuondoka hotelini walikofikia na
kwenda Mina (jiji la mahema) na kulala hapo tayari kwa siku inayofuata ya kisimamo cha Arafat. Eneo la Mina lipo
kilometa nane kutoka Msikiti Ni kazi ngumu kuepuka vifo kwa mahujaji Saud Arabia Mkuu wa Makkah na kilometa 14 kwenda viwanja vya Arafat.

Baada ya kushinda kutwa nzima kwenye viwanja vya Arafat, mahujaji wote huanza safari ya kwenda Muzdalifa ambako kuna umbali wa kilometa tisa, ili kuwahi kuswali sala ya Magharibi na Inshaa. Hapa ndipo misafara mikubwa ya mahujaji kuelekea upande mmoja huanza. Mahujaji wengine hutembea kwa miguu,
wengine hupanda hadi juu ya mabasi ili kuwahi kufika Muzdalifa, msongamano huu huwa ni hatari mno.

Nafuu kubwa ya msafara wanmahujaji kuelekea Muzdalifa huwa hakuna joto kali kama lile la mchana, kwa vile safari hii huanza jioni wakati jua limepoa lakini hata hivyo, watu karibu milioni mbili kuelekea upande mmoja na eneo moja huku kila hujaji akiwa na haraka zake za kufika huko, huwa ni kazi ngumu na ya hatari.

Mahala hapa mahujaji baada ya kuswali Magharibi na Inshaa, huokota kokoto 49 na hulazimika kuondoka usiku huo
kurudi Mina na baadaye kwenda kufanya Tawaf ya pili kwenye Msikiti Mkuu wa Makkah. Baada ya hapo hurudi tena Mina kwa ajili ya kusubiri zoezi la utupaji mawe linaloanza asubuhi ya siku inayofuata.

Zoezi la utupaji mawe huwa ni la siku tatu, siku ya kwanza kila hujaji hutakiwa kutupia mawe saba katika mnara wa kwanza. Mahujaji wote iwe wanaotumia njia ya chini inayounganisha Jamarati na mahema ya Mina au njia ya juu hupaswa kuingia eneo hilo kwa barabara pana mno yenye umbo la upinde iliyopo mashariki.

Mara zote katika zoezi la kutupia mawe katika minara hiyo, mahujaji hupaswa kutokea upande wa Magharibi ambapo kuna milango mingi yenye kuelekeza mahujaji maeneo yao walipofikia.

Mahujaji husaidiwa na ngazi za umeme zinazowawezesha kutoka eneo hilo haraka ili kuondoa msongamano wa mahujaji.

Katika siku hiyo ya kwanza, zoezi la utupaji mawe kwenye mnara huo wa mwanzo huambatana na kunyoa nywele
ambapo hufanyika nje ya Jamarati na mahujaji wafikapo kwenye mahema yao huwa huru, huvua rasmi mavazi ya
hijja Ihram na kuvaa nguo zao za kawaida kungojea siku inayofuata ambapo kila hujaji hurudi tena kupiga minara yote mitatu kila mnara mara saba.

Siku ya mwisho Jamarati hufunguliwa saa sita mchana na mahujaji hutakiwa kumaliza zoezi hilo kwa kumpiga shetani kwa kupiga minara yote mitatu kila mmoja mara saba kabla ya Jamarati kufungwa nyakati za jioni. Mahujaji hutakiwa kuondoka Mina kurudi mahotelini kuashiria kumalizika kwa ibada hiyo.

Jamarati ipo Magharibi mwa Mahema ya Mina, jiji hilihumeza mahujaji wote hivyo, kuna mitaa na barabara zinazo
unganisha mahema hayo na Jamarati. Inasemekana kuwa kufungwa kwa mtaa 206 upande wa mashariki ulikuwa chanzo kilichosababisha mahujaji waende kushoto mtaa wa 223 na kukutana na wenzao waliokuwa wanatoka mtaa wa 204 unaounganisha Mina na Jamarati.

Hali hiyo husababisha msongamano kwa kuwa huwezi kurudi nyuma kwa vile wale wa nyuma nao wanasonga mbele.
Mazingira haya husababisha majanga. Saudi Arabia ni nchi ya Jangwa, msongamano unapotokea ni lazima mahujaji
waanguke kutokana na joto kali. Hasa ikizingatiwa mahujaji wengi huwa na umri mkubwa na wengine huwa na maradhi ambapo wanapopata mshtuko kidogo hupoteza fahamu na kukanyagwa.

Licha ya Serikali ya Mfalmewa Saudi Arabia kutumia mabilioni ya fedha kujenga miundombinu ya kuifanya ibada
hii kuwa salama zaidi, bado kuna changamoto nyingi zinazopaswa kushughulikiwa siyo na serikali ya Mfalme wa Saudi Arabia bali pia na wadau wote wa Ibada za haj ili ibada iwe salama.

Changamoto ya kwanza inayoweza kusababisha vifo wakati wa ibada ya hijja ni mihemko ya waumini. Maeneo ambayo waumini hupagawa ni wakati wa kuzunguuka Al Kaaba. Hakuna idadi maalumu ya watu wanaopaswa kuingia kwa wakati mmoja, wengi wao hupenda kuzunguka pale chini hadi waiguse kaaba. Mahali hapo ni hatari mno, ukiteleza ukaanguka huwezi kupona kutokana na msongamano wa watu. Licha ya kujengwa kwa njia za ghorofa ambazo mahujaji huzunguka kwa nafasi na amani, mahujaji wengi hawataki kutumia njia hizo na hivyo kuwafanya maaskari wa Saudi Arabia kuwa na kazi ya ziada kuzuia watu.

Kudhibiti misongamano ya mahujaji mahali hapo inawezekana kwa kuwa kila kipindi cha ibada kinapofika mahujaji wote hutolewa nje ya eneo hilo hadi ibada inapomalizika. Hivyo hivyo inawezekana idadi ya mahujaji wanaweza kuingia mahali hapo kwa wakati mmoja kutawaf na kuondoka mara wamalizapo.

Mahali pengine ni Jamarati, kitendo cha kupiga mawe kila mnara hakichukui dakika moja kwa kila mnara na kusonga mbele, lakini mihemko ya mahujaji huwafanya wengine washindwe kutupa mawe na kusubiri wababe wamalize, mahujaji wengine badala ya kuondoka huanza kusoma dua ndefu mahali hapo.

Wengine husimama kuwasubiri wenzao na baadhi yao hupongezana. Wengine hutaka kutumia muda huo kupiga picha za kumbukumbu wakati wenzao wengi wapo nyuma wanakuja kufanya zoezi hilo. Pamoja na askari kuwafukuza ili waondoke, lakini mahujaji huwa wakaidi mno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles