23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Ni hatari kufungua soda kwa meno

GLORY LYAMUYA (DSJ) na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

JAMII imeshauriwa kuacha tabia ya kufungua vizibo vya chupa kwa kutumia meno kwa kuwa husababisha magonjwa ya kinywa na uharibifu wa meno.

Pia jamii inashauriwa wasitumie miswaki  ambayo brashi zake zimechakaa kwa kuwa nazo huharibu afya ya meno.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno (TDA), Gemma Berege alisema vitendo hivyo ni hatarishi kwa afya ya kinywa na meno.

Alisema kumekuwapo na tabia miongoni mwa  wanajamii kutumia meno kama kifaa cha kufungulia chupa za vinywaji na kusababisha meno kuvunjika.

“Pia waepuke matumizi ya sigara, tumbaku na unywaji wa pombe kupitiliza pamoja na kusafisha kinywa kwa kutumia mkaa huchubua fizi na kuharibu afya ya kinywa,” alisema Dk Gemma.

Aidha Dk Gemma alishauri jamii  kutumia dawa ya meno yenye madini ya floride kwa sababu madini hayo ni muhimu kukinga magonjwa yanayotoboa meno.

“Niwaombe Watanzania kujenga desturi ya kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno angalau mara moja kwa kila mwaka,”alisema Dk Gemma.

Aliongeza kuwa kwa watoto wadogo wanatakiwa kuchunguzwa afya hiyo mara mbili kwa mwaka ili kuwa na kinywa imara.

Daktari huyo alishauri pia jamii isisite kuhudhuria kliniki za matibabu ya afya ya kinywa na meno pindi  wanapogundua wana matatizo hayo.

Ushauri huo umejiri ikiwa Tanzania imeungana na dunia kusherehekea siku ya afya ya kinywa na meno ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 20 kila mwaka.

Maadhimisho hayo hapa nchini yalianza Machi 14, mwaka huu na kukamilika Machi 20 ambapo sherehe za kilele zilifanyika mkoani Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles