26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Array

NHC yaanza uhakiki wa wapangaji

MWANDISHI WEYU

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limeanza uhakiki wa wapangaji wake nchi nzima ili kuweka sawa taarifa za wapangaji wake kwa lengo la kubaini wapangaji wasio waaminifu.

Wapangaji hao, wanadaiwa wamekuwa wakiwapangisha wananchi wengine nyumba za shirika kinyume cha taratibu na kuwatoza kodi kubwa, huku wakijinufaisha na nyumba hizo.

Kwa mujibu wa tangazo la shirika hilo kwa umma, jana, lisema linawakaribisha wananchi wote wenye taarifa za wapangaji wanaojinufaisha na nyumba za shirika kutoa taarifa za wapangaji hao, makao makau au ofisi za shirika zilizoko katika mikoa mbalimbali nchini.

“Wananchi wanaopangishwa kinyemela na wapangaji wa nyumba za Shirika watakaotoa taarifa hizo watapewa fursa ya kuwa wapangaji wa nyumba hizo.

“Shirika linawaomba wapangaji wote kufuata taratibu za upangaii wa nyumba za shirika ambazo kimsingi ni mali ya umma na kwamba shirika halitasita kuwachukulia hatua kisheria ikiwemo kuwanyang’anya upangaji watakaokiuka taratibu za upangaji,” ilieleza taarifa hiyo ya Kitengo cha Huduma kwa Jamii cha NHC.

Hatua hiyo ,ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye Novemba 26, mwaka huu, aliagiza shirika kuhakikisha linafanya uhakiki wa nyumba zote zinazomilikiwa na shirika hilo ili kubaini wapangaji halali na wasio halali.

Lukuvi aliagiza uhakiki huo ufanyike nyumba kwa nyumba, mlango kwa mlango ili kubaini undanganyifu unaofanywa na wapangaji, ikiwemo katika majengo yenye maduka kwenye miji mikubwa.

Waziri huyo pia aliagiza uhakiki wa nyumba zilizotaifishwa na kukabidhiwa kwa Msajili wa majumba ambazo baadaye zilirejeshwa kwa wahusika kwa minajili ya ‘huruma’,  kuwa waishi hadi watakapofariki dunia, huku nyumba hizo zikiendelea kuwa mali ya Serikali.

Pia, aliagiza kupitiwa upya kwa miradi 192 ya ubia baina ya NHC na watu binafsi, akiitaka Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti kuangalia nmna ya kuboresha mikataba, ili shirika hilo linufaike na miradi hiyo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Novemba 26, Waziri Lukuvi alisema amechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa kumekuwa na udanganyifu miongoni mwa wapangaji wa nyumba hizo na wale waliowahi kupewa nyumba zilizokuwa zimetaifishwa, hivyo wanahitaji kuchukua hatua kudhibiti hali hiyo.

Alisema wizara yake imeona ni vyema uongozi wa NHC uanze uhakiki wa wapangaji wake kwa njia ya kielektroniki baada ya kubaini kuwa taarifa za wapangaji wengi hazipo kutokana na matumizi ya mfumo wa kizamani wa karatasi.

“Pitieni upya mikataba yenu na wapangaji. Kuna watu wameanzisha vishirika ndani ya shirika. Wanauza nyumba na kupokea wapangaji wapya. Kuna watu wanaopangisha nyumba lakini wenywewe hawapo, waliopo ni wengine kabisa, kwa hiyo tunahitaji uhakiki huu ufanyike.

“Tena katika uhakiki huu, muanzishe mfumo wa kielektroniki ambao utahusisha moja kwa moja taarifa zao na zile za vitambulisho vya Taifa vya Nida, kila mpangaji anapoingia kwenye nyumba ajulikane alikotokea na hata anakofanya kazi,” alisema.

Alisema katika uhakiki huo, wapangaji wote walioingia NHC kama wapangaji waliotozwa fedha zisizokuwa halali wajitokeze kwa kufika ofisini kwake na kuwasiliana naye naye atahakikisha wanarudishiwa fedha zao zote.

 “Ninawahakikishia, yeyote aliyetoza fedha kwa ajili ya kupata nyumba NHC kinyume na utaratibu, akija kwangu na vielelezo, nitahakikisha anarudishiwa fedha zake zote. Hata kama ikiwa ni shilingi milioni 40, ninajua zitakapopatikana, wahusika watazitapika,” alisema.

Alisema hakuna mteja atakayelazimishwa kulipa kodi kwa aidha mkupuo wa mizi mitatu, sita au mwaka, labda kwa maombi yake na ridhaa na hiyari yake mwenyewe.

Watendaji NHC

Akizungumzia utekelezaji wa uhakiki huo, Lukuvi alisema ana uhakika kuwa hautafanikiwa iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa, kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wa shirika hilo ambao walihusika kwa namna moja au nyingine katika udanganyifu, ambao watataka kuzuia kubainika.

Alisema ili kuhakikisha kuwa uhakiki huo unakua na ufanisi, anaagiza uongozi wa juu wa juu wa NHC chini ya Mkurugenzi Mkuu, Maulidi Banyani kuondoa wafanyakazi wote waliopo katika maeneo ya miji mikubwa na kuweka wengine.

“Kama hapa Dar es salaam, Mameneja wote waliopo wanatakiwa waondolewe kwa ajili ya uhakiki, wapelekwe sehemu nyingine. Waondolewe hapa waletwe wengine kwa ajili ya uhakiki. Siyo mameneja tu, kuanzia wale maofisa wa chini.

Hii inatakiwa kuwahusisha hadi maofisa wadogo kwa sababu hawa ndio wanaoweza kuchomoa mafaili na kuyapoteza, wanaweza kuchngia kukwamisha uhakiki,” alisema.

Majengo ya Msajili

Lukuvi alisema aliamua kuagiza uhakiki wa majengo yote yaliyotaifishwa na kuwekwa chini ya Msajili wa Majumba, baada ya kubaini kuwa kuna mchezo mchafu unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu kwa kushirkiana na wanasheria na hata watumishi wa shirika hilo.

Alisema alifanya ziara ya kushtukiza katika nyumba moja, yenye namba 43 iliyopo Kinondoni Ursino ambayo ilikuwa cini ya utaratibu wa msajili, ambayo kwa kuanzia tua walikuta ina mashaka katika umiliki wake.

“Nyumba hii ni miongoni mwa zile zilizotaifishwa lakini mmiliki alipewa aendelee kuishi mkwa misingi ya huruma, hadi atakapokufa. Makubaliano ni kwamba atakapokufa nyumba hiyo inarudi kwa Serikali, na nyumba hiyo alipewa muhindi lakini tumekuta inamilikwia na mghana.

“Kwa hiyo, ninawaagiza waangalie nyumba hizo zote na kujiridhdisha. Yeyote aliyenunua nyumba hizo kutoka kwa watu aliokuwa wamepewa au, mmiliki aliyekufa, au kwa ujanja ujanja, tunamfuatilia na hati zake zote ni za Serikali,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles