24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NHC Mbeya yatakiwa kuhamisha wapangaji kwa uchafuzi mazingira

Kenneth Ngelesi -Mbeya

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya imelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapa kuwaondoa wapangaji wote katika jengo la sinema, lililopo katikati ya jiji kutokana na shirika hilo kushindwa kuweka miundombinu ya maji taka hali inayosababisha maji machafu kutiririka ovyo mitaani na kuhatarisha afya za wananchi.

Jengo hilo lenye ghorofa moja ambalo ni mali ya NHC lilipo Mtaa wa Lupa, mkabala na Posta, katikati ya jiji la Mbeya, lina wapangaji zaidi ya 15, lakini halina mfumo wa maji taka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Ofisa Afya Kata ya Sisimba, John Oden alisema hali hiyo inasababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na maji taka kutiririka ovyo mitaani na ndiyo maana Halmashauri ya Jiji la Mbeya imelitaka shirika hilo kuondoka wapangaji hadi pale wakapoweka mfumo wa maji taka ndipo wawarudishe.

“Tunaenda kuwaandikia barua NHC waondoe wapangaji katika jengo hili, tunachukua hatua hii kwa lengo la kunusuru afya za wananchi na wapangaji pia,” alisema Oden.

Mmoja wa wapangaji wa jengo hilo, Dk. Briton Ngowi alisema kuwa kukosekana kwa miundombinu ya maji taka kwenye jengo hilo ni hatari kwa maisha yao sambamba na kuwakosesha wateja kwenye biashara zao kutokana na harufu kali katika jengo hilo.

“Hali siyo nzuri kwani mimi hapo nina kliniki ya meno, hivyo nimeanza kukosa watej,a hali siyo nzuri hivyo tungeomba waharakishe kuboresha miundombinu ya maji taka,” alisema Dk. Ngowi. 

Alipotafutwa Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya, Said Bundala alisema tayari wameshachukua hatua kwa kulipia gharama za uwekaji wa mfumo wa maji taka katika jengo hilo, lakini Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya ndiyo inayosuasua kufanya kazi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles