26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Nguli wa muziki wa Jazz, Oliver Mtukudzi amefariki dunia

Harare, Zimbabwe

Mwanamuziki nguli wa muziki wa Jazz kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ‘Tuku’ amefariki dunia katika hospitali ya Avenues mjini Harare nchini Zimbabwe alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mutukudzi amefariki akiwa na umri wa miaka 66 leo Jumatano Januari 23, taarifa za kifo chake zimetangazwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo.

Mwanamuziki huyo aliyekuwa na ziara za kimuziki katika nchi mbalimbali duniani, ilimlazimu kuzikatiza sababu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Amefariki ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha gwiji mwingine wa muziki wa Jazz, Hugh Masekela kutoka nchini Afrika Kusini, amefariki akielekea kuwa na miaka 67 na akiwa katika maandalizi ya albamu yake ya 67.

Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani, amekuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miongo minne, na amefanikiwa kutoa albamu 66.

Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa akipewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii wengine wengi kutoka nchi mbalimbali barani hapa ambao muziki wao umeleta hamasa kwa jamii.

Mutukdzi amezaliwa mnamo Septemba 22 mwaka 1952 mjini Harare Zimbabwe na katika uhai wake mbali na uanamuziki alikuwa pia mfanyabiashara, mhisani kwa watu wasiojiweza na Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto duniani (UNICEF) kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

Mara baada ya taarifa za kifo chake Mutukudzi kusambaa, wasanii wenzake na mashabiki wake wametuma salamu zao za rambirambi katika mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles