30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ngoma kutimka Yanga

ngoma*Wamisri wafika dau wataka waondoke nae

*Yanga yasema wakija mezani wanamuuza

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI hatari wa Yanga, Donald Ngoma, huenda akatimka katika klabu hiyo iwapo uongozi wa klabu hiyo utafikia makubaliano na klabu mbili za nchini Misri, zinazomtaka kwa udi na uvumba.

Klabu za Al Ahly na Zamalek, zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambae anang’ara na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ngoma ambaye amebakiza msimu mmoja wa kuitumikia timu ya Yanga, inadaiwa tayari ameanza mazungumzo ya awali na klabu ya Al Ahly.

Mzimbabwe huyo aliwavutia viongozi wa timu hizo, pale alipoonyesha kiwango cha juu katika mechi za Klabu Bingwa Afrika, kati ya Yanga na Ahly katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo wa marudiano Alexandria Misri, mchezaji huyo alionyesha kiwango kizuri na kufunga bao la kufutia machozi, kiwango ambacho kiliwavutia pia wapinzani wa Ahly Zamalek, mchezo huo uliisukuma Yanga nje ya michuano baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 hivyo kutoka kwa jumla ya bao 3-2 na kushuka kombe la Shirikisho.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro alisema kwa sasa wanachosubiri ni ofa kutoka kwa klabu hizo.

“Ni kweli tuliongea na wawakilishi wa timu hizo, ambao walionekana kumuhitaji mshambuliaji wetu na wameahidi kuleta ofa ndani ya wiki moja, kila kitu kitakuwa wazi endapo klabu hizo zitaweka fedha mezani kwa kuwaYanga ipo tayari kwa biashara hiyo,” alisema Muro.

Akizungumza na mtandao wa KingFut jijini Cairo, juu ya kujiunga Al Ahly, Ngoma alidai kuwa yupo tayari kujiunga na timu hiyo itakapowasilisha ofa kwa Yanga.

“Ndio nilizungumza nao siwezi kukataa, hata hivyo napata wakati mgumu kuchagua kwa kuwa zote ni timu kubwa Afrika,” alisema Ngoma.

Mbali ya Ngoma kuwa hatari katika michuano ya Kimataifa, mchezaji huyo ambae amecheza Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa mara ya kwanza ametikisa katika safu ya ufungaji bora, ambapo amemaliza ligi hiyo akiwa nafasi ya tatu akiwa na mabao 17. Amis Tambwe anaongoza safu hiyo akiwa na mabao 21 akifuatiwa na Mganda Hamjs Kiiza mwenye mabao 19.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles