23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

NGOMA AACHWA SAFARI YA AZAM UGANDA

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM              |      


TIMU ya Azam jana iliondoka nchini kwenda Uganda, lakini katika safari hiyo halikosekana mshambuliaji Donald Ngoma.

Ngoma aliyesajiliwa Azam kwa ajili ya msimu  ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea Yanga, amepewa mapumziko maalumu na klabu yake hiyo mpya kutokana na kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu.

Ngoma imeelekea  Uganda kama ambavyo imekuwa ikipendelea kufanya hivyo kila mwaka, kwa aajili ya  kupiga kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza kutimua vumbi Agosti 22.

Meneja wa Azam, Phillip Alando, aliliambia MTANZANIA jana kuwa, wakiwa Uganda wanatarajia kucheza michezo mitatu ya kirafiki ya kujipima nguvu na timu za huko.

Alizitaja timu wanazokusudia kucheza nazo michezo ya kirafiki kuwa ni Vipers SC, KCCA na Express FC.

“Tunaaamin kambi ya wiki mbili nchini Uganda itakuwa na faida katika kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Mchezaji ambaye hataambatana na timu ni Donald Ngoma,lakini waliosalia wote wanakwenda na timu Uganda,”alisema Alando ambaye pia  ana taaluma ya ualimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles