27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NGAWAIYA AWATETEA WASICHANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Cegodeta, Thomas Ngawaiya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Cegodeta, Thomas Ngawaiya.

Na SAFINA SARWATT- MOSHI

TAASISI ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (Cegodeta), imeishauri Serikali ichukue hatua zinazolenga kufanikisha utoaji wa elimu kwa watoto wa kike wanaopata ujauzito na kujifungua kabla ya kuhitimu masomo yao.

Aidha, taasisi hiyo imeunga mkono mijadala mbalimbali inayoendelea nchini ikiwamo inayoendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), juu ya kumsaidia mtoto aliyepata mimba akiwa masomoni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Cegodeta, Thomas Ngawaiya, alisema taasisi yake imeamua kutoa ushauri huo kwa kuwa imefanya utafiti na kugundua changamoto mbalimbali zinazohitaji utatuzi wa haraka.

Katika taarifa mazungumzo yake hayo, Ngawaiya alisema taasisi yake imeona kuna umuhimu wa Serikali na wadau wa elimu nchini kuweka mpango wa ujenzi wa madarasa na shule maalumu kwa ajili ya wanafunzi waliopata ujauzito na kujifungua ili waweze kuendelea na masomo.

“Hatua hiyo itawawezesha wale waliokumbwa na mikasa ya ujauzito, kurejea shuleni na pia itakuwa ni fursa nyingine ya kupata elimu ya malezi ya watoto wao.

“Ili mtoto huyu aliyejifungua arudi shuleni kuendelea na masomo ni vema kuwe na madarasa maalumu kwa ajili hiyo tu.

“Au ijengwe shule moja moja kwa kila wilaya, zikiwalenga watoto hawa ili waweze kupata masomo ya ziada ya malezi ya mtoto,” alisema Ngawaiya.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mbali ya utekelezaji wa mkakati huo, pia kumekuwa na changamoto ya mgongano wa kisheria unaosababisha kuwanyima haki watoto wenye umri chini ya miaka 18, hivyo akashauri suala hilo nalo litupiwe macho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles