NEYMAR AMTAKA PAULINHO KUTUA BARCELONA

0
949

BARCELONA, HISPANIA


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Barcelona, Neymar de Santos, ameanza kumshawishi kiungo wa klabu ya Guangzhou Evergrande ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini China, Jose Maciel ‘Paulinho’ kutua katika kikosi hicho cha nchini Hispania.

Kiungo huyo amehusishwa na kutaka kuondoka kwenye Ligi hiyo ya nchini China, hivyo Neymar amekuwa akifanya mazungumzo ya mara kwa mara, huku akimwambia kwamba Barcelona ni sehemu sahihi kwake.

Paulinho amekuwa na kiwango cha hali ya juu kwenye Ligi nchini China tangu alipoondoka kwenye kikosi cha Tottenham nchini England, hivyo mapema mwaka huu aliweka wazi kuwa muda wake umefika wa kutafuata sehemu nyingine ya maisha ya soka.

Neymar na Paulinho wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil, hivyo Neymar anaamini rafiki yake huyo akitua Barcelona atakuwa na jina kubwa kama ilivyo kwa viungo wengine.

“Uwezo wa Paulinho kwa sasa ni mkubwa sana, nimekuwa na uhusiano nzuri na nimejaribu kuzungumza naye juu ya kujiunga na Barcelona, ninaamini kila klabu kwa sasa inahitaji huduma ya mchezaji huyo na huu ni wakati wake wa kufanya maamuzi sahihi.

“Mchango wake nimeuona kwenye timu ya Taifa wakati wa michezo mbalimbali, ninajaribu kufanya mazungumzo na viongozi wa Barcelona ili kuona kama atawafaa,” alisema Neymar.

Paulinho tangu ajiunge na Guangzhou Evergrande mwaka 2015 akitokea Tottenham, amefanikiwa kufunga mabao 15 katika michezo 58 aliyocheza kwenye michuano mbalimbali, wakati huo akifunga mabao manne katika jumla ya michezo saba aliyocheza ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here