23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Neymar akutwa na virusi vya corona

PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Paris Saint-Germain, Neymar de Santos, ameripotiwa kukutwa na virusi vya corona pamoja na wachezaji wengine watatu.

Hata hivyo Paris Saint-Germain ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Ufaransa na kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameshindwa kuwaweka wazi wachezaji hao wengine ambao wamekutwa na virusi hivyo.

Lakini Angel Di Maria mwenye umri wa miaka 32 na Leandro Paredes mwenye miaka 26, wanatajwa kuwa kati ya wachezaji hao kwa mujibu wa L’Equipe.

Mara baada ya Paris Saint-Germain kumaliza mchezo wa mwisho wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Agosti 23, wachezaji hao watatu walionekana kuwa pamoja kwenye visiwa vya Ibiza wakiponda raha ambapo ni Neymar, Di Maria na Paredes.

“Wachezaji watatu wa Paris Saint-Germain wamethibitika kuwa na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo, hivyo hatua za kiafya zimeanza kuchukuliwa mara baada ya majibu hayo, lakini bado wachezaji na viongozi wengine wataendelea kufanyiwa vipimo kwa siku zinazofuata,” ilithibitisha timu hiyo kwenye mitandao yao ya kijamii.

Wachezaji wote watatu wametakiwa kukaa karantini kwa siku 14 huku wakiangaliwa afya zao. Ligi Kuu Ufaransa tayari imeanza kutimua vumbi huku Paris Saint-Germain wakitarajia kuanza kutupa karata yake ya kutetea ubingwa Septemba 10, mchezo huo utapigwa ugenini dhidi ya Lens.

Kutokana na hali hiyo, wachezaji hao watatu wataukosa mchezo wao wa kwanza na ule wa wapili dhidi ya Marseille ambao utapigwa Septemba 13.

Wachezaji hao watatu wa Paris Saint-Germain sio majina pekee ya wachezaji wakubwa barani Ulaya kukutwa na maambukizi hayo wiki za hivi karibuni, kiungo wa timu ya Manchester United, Paul Pogba, kiungo wa Tottenham, Tanguy Ndombele na wengine kama vile nyota wa Chelsea, Mason Mount, Tammy Abraham, Christian Pulisic na Fikayo Tomori wanatajwa kuwa na maambukizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,642FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles