Neymar ajiuzulu unahodha timu ya taifa

Neymar de Santos
Neymar de Santos
Neymar de Santos

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar de Santos, amechukua maamuzi ya kujiuzulu unahodha wa timu hiyo mara baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Olimpiki.

Katika michuano mbalimbali iliyopita, mchezaji huyo alikuwa anaonekana kuwa hana mchango na timu yake ya taifa na kudaiwa kuwa hana nidhamu, lakini katika michuano hiyo ya Olimpiki ambayo imemalizika juzi nchini humo, alitoa mchango mkubwa na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa huo ambao mastaa wengi wa nchi hiyo hawakufanikiwa kuupata.

Tangu kuanza kwa michuano hiyo Agosti 5 mwaka huu, nyota huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Barcelona, alipewa jukumu la kuwaongoza wachezaji wenzake kama nahodha, lakini baada ya kutwaa ubingwa ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

“Kuanzia sasa najiuzulu unahodha katika timu hii ya taifa, natarajia kumtumia ujumbe kocha wangu, Adenor Bacchi ‘Tite,’ kwamba kuanzia sasa afanye mpango wa kumtafuta nahodha mwingine.

“Nina furaha kubwa ya kuifikisha timu sehemu ambayo kila mmoja alitamani kuiona, ninashukuru nimefanikiwa kuiongoza hadi kutwaa ubingwa nikiwa nahodha na sasa ni wakati wa kuachana na nafasi hiyo na kuwapisha wengine watoe mchango wao,” alisema.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kuwa ubingwa huo kwake unamfanya ajisikie mfalme kwa taifa lake japokuwa kulikuwa na maneno kutoka kwa mashabiki.

Timu hiyo imetwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Ujerumani baada ya kutoka sare ya 1-1 dakika 90.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here