31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Neymar aiokoa PSG jua la jioni

PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa timu ya PSG, Neymar Jr, juzi aliungana na timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu na kufanikiwa kuifungia bao la pekee katika dakika za lala salama kwenye mchezo dhidi ya Strasbourg.

Neymar alikuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi pamoja na kushinikiza kutaka kuondoka kwa matajiri hao.

Neymar aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa timu hiyo hivyo mashabiki na viongozi walifikia makubaliano ya mchezaji huyo kuondoka, lakini hadi dirisha la usajili ilinafungwa Septemba 2, hakuna timu ambayo ilifikia makubaliano na uongozi wa PSG juu ya uhamisho huo.

Mbali na kushindikana kwa uhamisho wake, bado mashabiki wanamtaka mchezaji huyo kuondoka, hivyo kwa mara ya kwanza tangu kufunguliwa kwa msimu mchezaji juzi alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha PSG ikiwa ni mchezo wao wa tano wa ligi.

Mchezo huo ambao PSG walikuwa nyumbani, ulionekana kuwa mgumu, lakini Neymar alifanikiwa kuifungia bao la ufundi wa hali ya juu huku zikiwa zimebakia sekunde mchezo huo kumalizika.

Muda mwingi mashabiki walikuwa wanamzomea mchezaji huyo kila akigusa mpira, wengine walionekana akiwa wamebeba mabango ya kumtaka aondoke, lakini kelele zao alizinyamazisha kwa bao la tikitaka na kuifanya PSG iondoke na pointi tatu.

“Kila mmoja anajua kwamba nilitaka kuondoka, niliweka wazi na sitaki nilizungumzia hilo kwa kuwa kuna watu nitawaumiza, lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa PSG na lengo langu ni kuwa na furaha nikiwa uwanjani.

“Niliweka wazi kuwa, sina chochote kwa PSG wala mashabiki, lakini kunizomea kwao ni mambo binafsi, lakini hayo yote yamepita na sasa tunaangalia mbele na hii ni mara ya kwanza na mwisho kuzungumzia suala la uhamisho wangu, ninachokiangalia sasa ni PSG, nitahakikisha ninarudi kwenye ubora wangu kwa ajili ya timu,” alisema Neymar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles