27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Newcastle, West Ham zamwania Samatta

NA MWANDISHI WETU

BAO la kichwa alilofunga nahodha wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne Novemba 5 mwaka huu wakati timu yake ya Genk ikifungwa 2-1, imewatoa udende Newcastle na West Ham.

Kwa mujibu wa BBC Sport, Newcastle na West Ham wameonyesha nia ya kumsajili Samatta ambapo inaaminika kwenye mkataba wake kuna kipengele cha kumruhusu kuondoka kwa pauni milioni 10 (takribani Shilingi bilioni 30)

Msimu uliopita, Samatta alitwaa Kiatu cha Dhahabu katika Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu Jupiler Pro League akifunga mabao 25 na msimu huu tayari ameshafunga mabao sita katika mechi 13 za ligi na mabao mawili Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Japo Newcastle na West Ham haiwezi kumhakikishia Samatta kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya au Ligi ya Europa, lakini atapata nafasi kucheza Ligi Kuu England kila wiki.

Klabu zingine za Ligi Kuu England ambazo awali zilionyesha nia ya kupata saini ya Samatta wakati wa dirisha la usajili Julai mwaka huu ni Brighton, Burnley na Leicester City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles