27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Newcastle imeziba midomo ya watu’

LONDON, ENGLAND

BAADA ya timu ya Newcastle United kufanikiwa kushinda ugenini dhidi ya Tottenham bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, kocha wa timu hiyo Steve Bruce amedai matokeo hayo yamefunga midomo ya watu.

Katika michezo miwili ya awali baada ya kufungua msimu mpya wa ligi, Newcastle United ilipoteza yote, wakwanza alipoteza dhidi ya Arsenal kwa bao 1-0, kabla ya kichapo kingine cha mabao 3-1 dhidi ya Norwich City.

Kocha huyo amedai kuifunga timu bora ambayo ilifika fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita ni jambo ya kujivunia kwa upande wao hasa wakiwa kwenye uwanja wa ugenini.

“Tunahitaji kupewa matumaini na ninwashukuru wachezaji kwa ushirikiano waliouonesha kwenye mchezo huo ambao ulikuwa mgumu, lakini hawakutaka tamaa baada ya kupoteza michezo miwili ya awali.

“Kuna watu walikuwa hawaamini kama tungeweza kutoka na pointi tatu kwenye mchezo huo kwa kuwa tulikutana na timu bora kwenye Ligi Kuu, lakini umoja na ushirikiano wa wachezaji umesaidia kupata matokeo.

“Baada ya kutuzomea kwenye michezo miwili iliopita sasa tumewafunga midomo yao, huu ni ushindi wetu wa kwanza, tunatarajia kuendelea kufanya hivyo kwenye michezo mingine inayofuata kikubwa ni kuendelea na kiwango walichokionesha wachezaji wangu,” alisema kocha huyo.

Bao hilo la Newcastle United lilifungwa na mshambuliaji wao mpya Joelinton de Lira ambaye amejiunga na timu hiyo wakati huu wa kiangazi akitokea klabu ya Hoffenheim kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 35.

Hilo lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunge huku akiwa tayari amecheza michezo yote mitatu ya Ligi Kuu England.

Bruce anaamini mchezaji huyo mpya raia wa nchini Brazil, ataisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika safu ya ushambuliaji baada ya kuwa na maelewano mazuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles