30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Netanyahu apingwa mahakamani

JERUSALEM, ISRAEL

MAHAKAMA ya Juu ya Isreal imesikiliza hoja za kumpinga Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika harakati zake za kutaka kuiongoza serikali ya muungano. 

Wapinzani wanasema kwamba makubaliano ya kuunda serikali mpya ya muungano yatamlinda kinyume cha sheria katika kesi ya ufisadi inayomkabili. 

Jopo la majaji 11 wa mahakama hiyo ya juu lilikutana kwa mara ya pili jana baada ya kusikiliza hoja nyingine juzi Jumapili dhidi ya mamlaka aliyopewa Netanyahu kuunda serikali licha ya kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi, udanganyifu na kukiuka uaminifu. 

Mahakama hiyo inatarajiwa kutowa uamuzi wake Alhamisi. 

Ikiwa itaamua dhidi ya Netanyahu, huenda uchaguzi wa nne wa mapema ukaitishwa nchini humo. 

Netanyahu na mpinzani wake mkuu, Benny Gantz walisaini makubaliano mwezi uliopita wa kuunda serikali ya muungano chini ya mfumo wa kubadilishana uongozi baada ya kushindwa kupatikana mshindi wa moja kwa moja katika chaguzi tatu zilizofanyika.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,352FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles