25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Netanyahu aondoa ombi la kinga dhidi ya mashtaka

Tel Aviv, Israel

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, jana ameondoa ombi lake la kinga dhidi ya mashtaka ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge.

Katika taarifa iliyotolewa katika ukurasa wake rasmi wa Facebook, Netanyahu aliyekuwa ziarani Washington kabla ya uzinduzi wa mpango wa amani wa Rais Donald Trump, alisema kuwa ameamua kutoruhusu mchezo huo mchafu kuendelea.

Bunge la Israel lilitarajiwa kuandaa kikao cha kuzungumzia kubuniwa kwa kamati ya kujadili ombi hilo la waziri huyo mkuu la kinga ya mashtaka dhidi yake.

Netanyahu alishtakiwa kwa makosa ya ulaghai, kuvunja uaminifu na hongo Novemba mwaka jana katika visa vitatu tofauti. Hata hivyo amekanusha mashtaka hayo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles