Neddy awaasa wasanii kutoa misaada hospitalini

0
1388


Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Msanii wa muziki wa ‘Bongo Fleva’ Said Seif maarufu ‘ Neddy Music’ amewaasa wasanii wenzake kutoa misaada katika hospitaIl mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 4, wakati akitoa misaada ya vitu mbalimbali katika hospitali ya Mwananyamala kitengo cha watoto jijini Dar es salaam, ambapo ametoa vyakula, dawa na vifaa tiba.

” Nimeamua kutoa misaada hii ya vitu hivi ili kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuona mwaka mpya tena na nitakuwa natoa misaada hii kila mwezi kwa kile ambacho Mungu ananiwezesha,” amesema Neddy.

Kwa upande wake Muuguzi wa hospitali hiyo kitengo cha watoto Elizabeth Sanga ameshukuru kwa kupokea misaada hiyo na kuwaomba wasanii wengine wajitokeze kwa wingi kwenye kutoa misaada hospitalini ili kuipiga tafu sekta ya afya.

“Ni wasanii wachache sana wenye moyo kama wa Neddy, wa kujitolea niwaombe tu wajitokeze kwani kutoa misaada ni njia ya kumshukuru Mungu kwa kutuvukisha kuuona mwaka mwingine, “amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here