25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NEC yatangaza uchaguzi Jimbo la Temeke

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam na kwenye kata 46 za Tanzania Bara.

Akitangaza uchaguzi huo Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage, amesema utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.

“Uteuzi wa wagombea utafanyika Desemba 20, mwaka huu, kampeni za uchaguzi zitafanyika kati ya Desemba 21, hadi Januari 18, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni Januari 19 mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.

Aidha, Jaji Kaijage amesema tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya ubunge katika jimbo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles