26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NECTA, Taasisi zaombwa kuhifadhi karatasi zilizotumika

Na Sarafina Swaratt, Kilimanjaro

Kiwanda cha karatasi cha China Paper Cooparation Compay Ltd cha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kimetoa wito kwa Taasisi za Serikali ikiwemo Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) kutunza karatasi zilizotumika na kuzipelekea kiwandani hapo badala ya kuzichoma moto.

Hatua hiyo inatokana na Kiwanda hicho kutumia karatasi katika uzalishaji bidhaa mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kiwandani hapo leo Alhamisi Mei 27, 2021, Meneja kiwanda hicho, Wilium Mbila amesema mali ghafi kubwa ya kiwanda hicho ni karatasi na kwamba wadau wake wakubwa ni NECTA pamoja na taasisi nyingine za serikali na benki.

“Sisi kama kiwanda tuna nunua karatasi zilizotumika na kuzalishia bidhaa kama karatasi laini (Tishu) ambazo zinatumika katika hoteli mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, hivyo tunatoa rai kwa taasisi hizo kwamba wasichome karatasi walete kiwandani kwani hatuchukui bure,”amesema Mbili.

Mbila amesema uwekezaji wa kiwanda hicho ni zaidi ya Sh bilion tano na kwamba taka zote zinazozalishwa zinatumika kuzalisha bidhaa.

Aidha, kiwanda hicho kinaiomba serikali kukipatia eneo kubwa la shamba la kupanda miti ya kutengeneza karatasi na bidhaa nyingine zinazotokana na miti.

Amesema hatua hiyo itasaidia kutunza mazingira kwa faida ya vizazi vijavyo na kwa sasa wananunua miti na magogo kutoka mashamba ya serikali yaliyopo West Kilimanjaro wilayani Siha, Rongai na Rombo.

Amesema pia wamekuwa wakinunua miti kwa wananchi na kwamba licha ya kuwepo kwa masoko ya bidhaa zao hapa nchini kuibuka kwa ugonjwa wa corona umeleta changamoto ya masoko duniani kote.

Mbali na kuzalisha karatasi laini (Tishu) kiwanda hicho pia inazalisha plywood ambazo zinatumika kujenga madaraja na majengo makubwa.

Baadhi ya wadau mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji ili viwanda vilivyokufa viweze kufufuliwa ili kuchochea ajira kwa vijana na kuongeza mapato ya serikali na wananchi kwa ujumla.

Miongoni mwa wadau hao ni Ngereza Mghamba ambaye amesema kuwa viwanda vingi Moshi havifanyi kazi na kwamba endapo serikali itavifufua viwanda hivyo itasdia kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira mitaani na kupunguza matukio ya kihalifu.

“Ombi langu kwa serikali ivilinde viwanda mabavyo bado vinafanya kazi huko ikiendelea kutafuta muafaka wa kukifufua vingine ili vijana tupate ajira tuweze kuendesha maisha,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles