27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NEC yawataka wasimamizi wa Uchaguzi kushirikisha vyama

Elizabeth Kilindi, Njombe.

KAMISHNA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Mary Longway, amewataka wasimamizi wa uchaguzi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kushirikisha vyama vya siasa na wadau katika maswala ambayo wanastahili kushirikishwa ili kuwa na uchaguzi huru na haki.

Kamishna Longway ameyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo kwa waratibu wa Mikoa, wasimamizi na wasimamizi wasidizi wa uchaguzi kutoka Mikoa ya Ruvuma, Iringa na Njombe ambapo alisema ni muhimu pia kuhakikisha wanayajua na kuyatambua vyema maeneo ya kufanyia kazi, miundombinu ya kufika katika kata na vituo vyote vya kupigia kura.

“Hawa kwa ngazi hii ya mkoa ndio wawakilishi wa tume ngazi ya mkoa na wao tunawapa semina hii ya majukumu yote na taratibu na hatua zote zinazotakiwa kuchukuliwa wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi mpaka kumalizika na matokeo yametolewa ili kama kuna kesi pia ziwe zimemalizika.

“Hivyo tumewapa shughuli zote ambazo Tume ingekuwepo sehemu zote za nchi hii ingeweza ikafanya na ndio maana kwa sababu tume hatupaswi kuwa na muelekeo wowote wa kisiasa inaweza kufanya kazi yake kwa weredi, inabidi kuwaapisha viapo vyote viwili vya kuondokana na chama chake kama anacho na kutunza siri,” alisema Jaji Mary.

Aidha, alisema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali ambazo zinapaswa kufutwa na kuzingatiwa hivyo kupunguza, kuondoa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

“Nasisitiza kwenu muhakikishe mnazingatia maelekezo mnayopewa na tume katika mafunzo badala ya kufanya kazi kwa mazoea pia muhakikishe mnafuata matakwa ya kikatiba,sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi yanazingatiwa wakati wote,” alisema Jaji Mary.

Naye, Afisa Msaidizi wa Uchaguzi jimbo la Lupembe, Lukelo Mshaura, alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika mchakato mzima wa uchaguzi uwe huru na haki kwa kufuata taratibu zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles