26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

NEC yaonya hakuna vituo hewa

Na RAMADHAN HASSAN – DODOMA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), imesema hakuna kituo wala mpiga kura hewa tofauti na waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hivyo kuwataka wote wenye ushahidi wa uwepo wa tuhuma hizo kuwasilisha ushahidi wao kinyume na hilo watachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yalielezwa jijini Dodoma jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi,Dk.Willson Mahera alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema taarifa hizo hazina ukweli

wowote, zinalengo la kuleta taharuki na kuchafua taswira ya tume.

Alisema mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ulianza kufanyika Aprili mwaka jana kwa kubainisha vituo vya kupigia kura na ulikuwa shirikishi kwa vyama vyote vya siasa.

Alitaja idadi ya vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura vilikuwa 37,814 na vituo vya kupigia kura ni 80,155, inatokana na kituo kimoja kilichotumika kujiandikisha kinaweza kutoa vituo vitatu kwa sababu kituo kimoja kinatakiwa kuwa na wapiga kura 450 hadi 500.

Aliwataka wagombea wa kiti cha urais

na makamu wa rais kuzingatia ratiba toleo la sita ya kampeni iliyotolewa na tume, ikiwemo kuheshimu kanuni,sheria na taratibu za tume kwa kumaliza mikutano kwa muda uliowekwa.

Alisema tume imejiandaa vizuri katika uchaguzi na tayari vifaa vyote muhimu vimeishafika majimbo ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Aliwataka wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kufikisha vifaa hivyo kuanzia jana kwenye vituo vya kupigia kura ili kusijitokeze dosari zozote. Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unatarajia kufanyika keshokutwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles