22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

NEC YAITAKA MAREKANI KUTHIBITISHA MADAI YAKE KUHUSU UCHAGUZI MDOGO

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam             |        


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekanusha taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani kwamba katika uchaguzi mdogo uliofanyika Agosti 12, mwaka huu uligubikwa na vurugu na uvunjifu wa sheria.

Aida, Tume pia imeutaka Ubalozi huo kuthibitisha wanachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 36.

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC iliyotolewa na Ofisa Habari Mwandamizi wa tume hiyo, Christina Njovu, imesema Ubalozi huo umetoa taarifa inayotoa tuhuma dhidi ya
Serikali, tume na Jeshi la Polisi kuwa sheria haikufuatwa na pia ulikuwa na vurugu katika uchaguzi huo.

“Uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa Kimataifa, je Ubalozi huo umetoa wapi taarifa hizo? Na hayo waliyoyaona, wameyaona
kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi?

“Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa Ubunge mmoja wapo kupitia Chadema alijitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kueleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo, na ameshukuru kwa kuwa Uchaguzi huo umemjenga.

“Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika mbo husika vinashughulikia.

“Aidha, tume inapenda kuufahamisha umma kuwa Tanzania ni nchi huru na inaendesha chaguzi zake kwa mujibu wa Katiba yake na Sheria za Uchaguzi. Kama kuna ambaye hajaridhika bado sheria za nchi zinampa fursa ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka mbalimbali zilizopo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,204FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles