33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

NEC kutoongeza, kupunguza majimbo ya uchaguzi

Mwandishi Wetu -Dodoma

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa haikusudii na wala haina mpango wa kuongeza au kupunguza majimbo ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu wa 2020.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dodoma na Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera wakati akijibu swali kutoka kwa Mtangazaji wa Clouds wakati akishiriki kipindi cha Clouds 360 kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja na kituo hicho kutoka katika ofisi mpya za Tume zilizopo eneo la Njedengwa jijini hapa.

Alisema kuwa hatua ya hivi karibuni ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya kufuta baadhi ya majimbo ya uchaguzi ililenga kuweka uwiano wa majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Zanzibar.

Dk. Mahera, alisema kuwa kutokana na ushirikiano wa tume hizo mbili wakati wa uchaguzi hivyo kufanya majimbo ya Uchaguzi Zanzibar kubakia 50 badala ya 54 ya awali.

 “Tume inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za Uchaguzi hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake tume inazingatia muda kadiri unavyoelekeza kisheria ikiwa ni pamoja na ratiba ya uchaguzi,” alisema Dk. Mahera.

Alipoulizwa kuhusu tume kuchelewa kutangaza tarehe ya uteuzi wa wagombea, Dk. Mahera  alisema kuwa tume itatangaza ratiba yote ya uchaguzi mara tu baada ya kutolewa kwa Tangazo la Serikali kuhusu kuvunja Bunge ambapo kwa mujibu wa Sheria si chini ya siku tano na si zaidi ya siku 25 baada ya tangazo hilo.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi ametoa rai kwa wananchi na hususan vijana na wanawake waliojiandikisha kuwa wapiga kura kujitokeza kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kushiriki katika kupiga kura Siku ya Uchaguzi itakapowadia kwani takwimu zinaonesha vijana wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles