22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

NDUMBARO AWATAKA WAGONJWA, WAUGUZI SONGEA KUTUNZA VIFAA TIBA

Na Amon Mtega, Songea

Mbunge wa jimbo la Songea Mjini Dk. Damas Ndumbaro (CCM), amewataka wauguzi na wagonjwa wanaopatiwa huduma za matibabu katika Kituo cha Afya cha Mjimwema kilichopo Manispaa ya Songea, kuvitunza na kuthamini vifaa vilivyotolewa na Rais John Magufuli ili viwasaidie kwa muda mrefu.

Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni vitanda 20, magodoro 20, vitanda vya kujifungulia wajawazito vitano na mashuka 50 vyenye thamani ya Sh 18.2, kwa niaba ya Rais Magufuli, Dk. Ndumbaro amesema vifaa hivyo vinatakiwa vitumike vizuri ili viweze kudumu kwa muda mrefu kwani havipatikani kiurahisi kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

“Vifaa hivi vigawanywe pia katika vituo vipya vya kutolea huduma kama vile Zahanati ya Lilambo B, Mahilo na Masigira ili nako visaidie kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolala chini katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea,” amesema.

Akipokea msaada huo Daktari wa Manispaa ya Songea Dk. Mameritha Basike amesema pamoja na msaada huo bado kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa gari ya kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi mashine ya Ultra Sound, X-ray mashine, mashine ya kufulia mashuka ya wagonjwa na kukosekana kwa duka la dawa la bima ya afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles