27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugulile: Baadhi ya NGOs zinatakatisha fedha

Na Anthony IshengomaDodoma

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, amesema Serikali haitazifumbia macho asasi za kiraia (NGOs) zinazojiingiza katika masuala yanayohatarisha usalama wa nchi au utakatishaji fedha. 

Ndugulile alisema hayo jana mjini Dodoma wakati akifungua mkutano wa NGOs ambapo ameyataka mashirika hayo kuepuka vitendo vya udanganyifu.

Dk. Ndugulile alisema kuna baadhi ya NGOS ambazo zinafanya kazi kwa udanganyifu bila kufuata katiba zilizowasilishwa wakati wa usajili wake.

Alisema kwa sasa zimejiingiza katika matendo yanayohatarisha usalama na kuonya Serikali haitakuwa tayari kuyapa nafasi mashirika kama hayo kufanya kazi Nchini.

Dk. Ndugulile aliyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuzingatii vipaumbele vya Taifa ili kuepukana changamoto ya mashirika mengi kufanya kazi katika eneo moja jambo ambalo linaacha maswali kwa kuwa Tanzania ni moja kwa nini mashirika mengi yanajielekeza na kutoa huduma sehemu fulani ya Nchi wakati kuna maeneo mengine ya kipaumbele yanakuwa hayana mdau wa NGOs hata moja.

Aidha amezitaka NGOs zote Nchini kuzingatia vipaumbele vya Serikali na kuacha tabia ya baadhi ya NGOs zinazoitaka Serikali kufuata matakwa ya NGOs hizo katika suala zima la mahali zinapotaka kufanya kazi.

Katika hotuba yake kwa Wajumbe wa Mkutano huo Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imekamilisha kanzidata ya NGOs zote Nchini lakini pia kuweka mfumo wa kielektroniki ili kuhakikisha taarifa zote za NGOS zinafika kwa wakati.

Aidha Ndugulile alizitaka NGOs kote nchini kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji kama ambavyo NGOs zimekuwa zikiitaka Serikali kutekeleza wajibu huo na kuziagiza kuhakikisha zinatangaza na kuweka wazi kiasi cha fedha wanazopata kutoka kwa wafadhili wao ili jamii na Serikali wajue matumizi ya fedha hizo lengo likiwa ni kushirikiana baina ya Serikali, wanufaika na Mashirika hayo.

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unaendelea Jijini Dodoma ambapo Naibu Waziri Ndugulile amewaambia Wajumbe wa Mkutano huo kuwa Serikali inaendelea kuboresha Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kutumia fursa hiyo kuwambia wajumbe hao kuhusu kukamilika kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mshirika hayo Dkt. Richard  Faustine Sambaiga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles