Ndugu kizimbani kwa unyang’anyi Kiteto

0
833

Mohamed Hamad, Kiteto

Ndugu wawili wa familia moja, Shadrack Simon (25) na Julius Simon (29), wakazi wa Kitongoji cha Nalang’tomoni Wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamefikishwa Mahakamani ya Hakimu mkazi wilaya ya Kiteto kwa unyang’anyi.

Akisoma shitaka hilo mwendesha mashtaka wa Polisi Mwandiba Wambura mahakamani hapo amedai mbele ya Hakimu Joakimu Mwakiyolo kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 20 mwaka huu kijijini hapo.

Amedai watuhumiwa hao kwa pamoja wakiwa Kitongoji cha Nalang’tomon Kiteto walimshambulia kwa silaha za jadi Abel Charles na kumpora Sh milioni 1.8.

Hakimu Mwakiyolo aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 12, mwaka huu kwaajili ya kutajwa huku watuhumiwa wakiendelea kuwa mahabusu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here