23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai: Viongozi wa serikali ongeeni ukweli mbele ya rais

AMADHAN HASSAN – DODOMA

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameeleza uwepo wa baadhi ya viongozi wa serikali kuthubutu kumdanganya hadharani Rais Dk. John Magufuli kuwa wabunge waliokwenda kuishangilia timu ya soka ya Tanzania “Taifa Stars” inayoshiriki michuano ya AFCON, kwamba waliwadhihaki wachezaji.

Spika ametoa kauli hiyo bungeni leo Juni 25, baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo), kuomba muongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7), kuhusu jambo lililotkea mapema bungeni.


Zitto alilazimika kuomba muongozo huo baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars baada ya mchezo wake na Senegal.


“Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema, umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.

Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu akisisitiza kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.


“Naomba tusilikuze jambo hili kabisa, kama wabunge tungekuwa na mawazo kama wachezaji wanamakosa isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki kumdanganya Rais hadharani.

“Kiongozi wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele ya Mwenyenyezi Mungu na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka kidogo…inatosha..inatosha.


“Nasema wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza kumtukana Spika, lakini tuache,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles