25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai mgeni rasmi Wiki ya Azaki, wananchi waombwa kujitokeza

Na Hughes Dugilo, Dar es Salaam

Katika kuelekea katika Wiki ya Azaki inayotarajiwa kuanza rasmi Oktoba 23, mwaka huu wadau mbalimbali wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo hususan wakazi wa Jiji la Dodoma na mikoa ya jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatatu Oktoba 18, kwenye Ofisi za Foundations For Civil Society (FCS) jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility Tanzania (LSF), Lulu Ng’wanakilala amesema kuwa mgeni rasmi katika Maonesho hayo anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility Tanzania (LSF), Lulu Ng’wanakilala (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya wiki ya Azaki yanayojarajiwa kuanza Oktoba 23, 2021 jijini Dodoma, (wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi ya TANGO, Ramadhan Masel, (wa tatu kushoto) ni Anna Henga Mkurugenzi wa kituo cha sheria LHRC, na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS,Francis Kiwanga.

Amesema kuwa Spika Ndugai ni kingozi anayesimamia Muhimili wa Bunge ambao ni muhimili muhimu kati ya mihimili ya nchi yetu nakwamba atapata fursa ya kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na Asasi za Kiraia ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni ”Azaki na Maendeleo”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TANGO, Ramadhan Masele amesema katika siku saba za maonesho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika Jijini humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundations For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa moja ya mambo ambayo yatafanyika ni utoaji wa msaada wa kisheria kwenye Mabanda mbalimbali lakini pia kutakuwa na utolewaji wa elimu kuhusu chanjo ya Uviko – 19.

Pia Oktoba 24, kutakuwa na mijadala mbalmbali ikiwano kuangalia namna ambavyo wanashirikiana na Serikali na mengine mengi yanayohusu maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Anna Henga Mkurugenzi wa kituo cha sheria LHRC amesema katika maonesho hayo kutakuwa na utoaji wa tuzo mbalimbali ikiwa ni eneo la jinsia, uwajibikaji kwa Jamii, walemavu, na mengineyo ambapo tuzo hizo zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima Oktoba 28, 2021.

Amefafanua kuwa kuna Asasi nyingi ambazo zinafanya kazi vizuri hivyo watatambua mchango wao katika maendeleo ya nchi kupitia wiki hiyo ya Azaki.

Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC), Anna Henga akizungumzia tuzo mbalimbali zitakazotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, Oktoba 28, 2021.

Akihitimisha mkutano huo na waandishi wa habari amesema Azaki watashirikiana na Sekta Binafsi kwenye nyanja mbalimbali, na kuwataka wadau na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga amesema kuwa wao kama Azaki wanatambulika na Serikali na wanapata ushirikiano mkubwa na chini ya rais Samia Hassan Suluhu kuna mwelekeo mzuri.

Amesema Kuwa katika maonesho hayo pia wanatarajia kujadili maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo aliyatoa kwao nahivyo sehemu ya maonesho hayo ni majadiliano.

Kiwanga meongeza kuwa katika maonesho hayo wamejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanapata faida kupitia wiki hiyo na katika hilo wanatambua umuhimu wa waandishi wa habari na ndio maana wamekuwa nao nyakati zote.

“Lengo letu kubwa nikuona kila kinachofanyika wananchi wanakipata na kinawafikia hivyo kutakuwa na jobo la waandishi kutoka Dar es salaam na wengine watakuwa wa Dodoma”amesema Kiwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles