26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai mgeni rasmi maadhimisho ya walemavu

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Watu wenye ulemavu duniani yatakayofanyika kimkoa Wilayani Kongwa.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (Shinyawata) Mkoa wa Dodoma, Justus Ngw’antalima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Katibu Mkuu huyo wa Shinyawata Dodoma, alisema kuwa mahadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Desemba 1 hadi 3 wilayani Kongwa mwaka huu.

“Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo kwa pamoja tunataka kupaza sauti kuhusiana na mambo ya watu wenye ulemavu,”alisema Katibu huyo.

Ngw’antalima alisema kuwa siku hiyo Spika wa Bunge atatumia nafasi hiyo kukabidhi vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu wa wilaya hiyo.

Katibu huyo alisema jumla ya washiriki 500 kutoka vyama mbalimbali vya watu wenye ulemavu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma wanatarajiwa kushiriki.

Katibu huyo alisema pamoja na kukabidhi vifaa, pia shughuli mbalimbali zitafanyika kwenye mahadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa watu watakaoshiriki.

Alisema kuwa miongoni mwa elimu itakayotolewa ni pamoja na jamii kuondokana na dhana ya mila potofu ya kuwabagua watu wenye ulemavu katika kupata elimu pamoja na fursa mbalimbali.

“Ni matengemeo yetu kuona watu wenye ulemavu wakipatiwa haki zao za kimsingi ikiwemo afya, elimu na haki sawa kama ilivyo kwa wengine ambao hawana ulemavu wowote, siku hii tutakutana kwa pamoja na kujadiliana maana sisi tuna shida nyingi ambazo zinahitaji msaada,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles