27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Ndugai awataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kujiepusha kutorosha madini nchini

Ramadhan Hassan,Dodoma

Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka wachimbaji na wafanyabishara wa madini kuyatumia masoko ya madini ambayo yameanzishwa hivi karibuni katika makao makuu ya kila mkoa na kujiepusha na tabia ya kutorosha madini pamoja na magendo.

Akizungumza leo Mei 26, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya madini katika viwanja vya bunge, Ndugai amesema wote wanaojishughulisha na biashara na uchimbaji wa madini kuyatumia masoko ya madini yaliyoanzishwa hivi karibuni.

‘Tumeshuhudia msisitizo unaoonyeshwa na Mheshimiwa Rais katika uanzishwaji wa masoko ya madini na yanafunguliwa kila mahali katika nchi yetu tukianzia na makao makuu ya kila mkoa.

“Kwahiyo ndugu zangu mnaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa ya madini na bishara ya madini yatumieni masoko hayo, jiepusheni na tabia ya kutorosha madini na magendo,”amesema Spika Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles