23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Ndugai awasisitiza Wakenya kujifunza zaidi Kiswahili

Anna Potinus

Spika wa Bunge, Job Ndugai amewasihi Wakenya kuongeza juhudi katika kujifunza lugha ya Kiswahili kwani kwa sasa ni moja ya lugha rasmi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kwamba itawasaidia kufanikiwa katika mambo mbalimbali.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo nchini Kenya wakati akizindua Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya kwa lugha ya Kiswahili na matangazo ya moja kwa moja ya bunge.

“Ukitaka kujifunza lugha fulani ni lazima utumie kamusi ya lugha yenywe, kwahiyo ninawatia moyo muendelee kujifunza Kiswahili kwasababu sasa hivi kinatumika kama alugha mojawapo muhimu na rasmi katika Jumuiya ya SADC, Umoja wa Afrika, Bunge la Afrika lakini pia kwenye Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kiswahili ni moja ya lugha rasmi inayotumika.

“Ili uweze kupata mafanikio ni vizuri ukajua lugha ya kiswahili hata kama ni kile cha kuombea maji, sio vibaya kuzungumza kiingereza lakini ili uweze kufanikiwa katika mambo yako unayoyafanya ni vyema ukajifunza Kiswahili pia,” amesema Ndugai.

Aidha amewapongeza kwa taarifa za kamati walizoziandaa na kwa hatua waliyoifikia ya kurusha mubashara matangazo ya kamati za bunge kwaajili ya wananchi wa Kenya kuona kinachoendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles