24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Ndugai aipongeza Simba kutetea ubingwa

Ramadhan Hassan,Dodoma

Spika wa Bunge Job Ndugai , ameongoza Wabunge kushangilia ubingwa wa timu ya Simba Sport Club leo Mei 22 mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Jana Simba Sc iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United mchezo uliofanyika katika uwanja wa Namfua Mkoani Singida hivyo kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni,Spika Ndugai amechombeza kwa kudai kwamba Ligi imeisha wale ambao wanaendelea kutafuta ubingwa na waendelee

“Jamani Ligi kuu inaendelea,wale ambao bado wanaendelea kutafuta ubingwa waendelee,Ligi bado haijaisha.

“Lakini kwa niaba ya Simba tuwapongeze sana Simba kwa kunyakua ubingwa 2019-2020,Hongereni sana Simba.

“Lakini pia niwapongeze sana watani wetu Yanga kwa kufanya juhudi ya kuongoza Ligi kwa muda mrefu.

“Na leo mtamuona Mheshimiwa Jenista Mhagama jinsi alivyopiga na ua lake lile,”amesema Spika Ndugai huku Wabunge wakishangilia.

Katika hatua nyingine,Spika Ndugai amempongeza Waziri Mkuu kwa kuipandisha timu ya Namungo Fc kutoka katika Jimbo lake.

Namungo ilikuwa ikishiriki Ligi daraja la kwanza na imefanikiwa kupanda daraja na msimu ujao itacheza Ligi kuu ya Tanzania Bara.

“Lakini Waheshimiwa Wabunge sijui kama mnafahamu kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu amepandisha timu ya Jimboni kwake kutoka kule walikokuwa

“Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakupongeza sana ni jambo kubwa timu zinazoingia kule kila watakapoenda Ruangwa wajipange kwahiyo tunakupongeza sana.

Pia Spika Ndugai amewataka Wabunge kuunga mkono michezo katika maeneo wanayotoka.

“Basi tuunge mkono michezo katika maeneo yetu kwa sababu michezo inasaidia kujenga umoja wa kitafa,”amesema Spika Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles