26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai aahidi kusaidia Mahakama kupata raslimali za kutosha

Mwandishi wetu- Dodoma

SPIKA Job Ndugai, amesema  Bunge litashirikiana na Serikali  kuhakikisha Mahakama inapata rasilimali za kutosha ili iweze kutekeleza  majukumu yake ya kutoa haki kwa wakati.

 Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya utoaji  elimu ya sheria iliyoambatana na   matembezi  maalum ya kilomita tano yaliyoanza kwenye viwanja vya Mahakama Kuu  Dodoma hadi viwanya vya Nyerere Square, Ndugai aliipongeza Mahakama kwa maonesho mazuri.

‘’Bunge litashirikiana na Serikali kuhakikisha  Mahakama inapata rasilimali za kutosha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki kwa wakati,’’ alisema Spika.

Aidha Spika Ndugai alitoa wito kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja hivyo ili wajue haki zao na kupata elimu ya sheria kwa kuwa Mahakama si sehemu ya kuogopwa.

Ndugai aliipongeza Mahakama kwa kauli mbiu yake ya mwaka huu inayosema ‘Uwekezaji  na Biashara: Wajibu   wa Mahakama na Wadau  kuweka Mazingira wezeshi ya Uwekezaji.’ Kwa kuwa inasaidia kufikisha dhamira ya Serikali  ya awamu ya tano kujenga uchumi imara  na viwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith  Mahenge, alitoa shukrani kwa Mahakama  kujenga majengo ya  Mahakama Jumuishi na  Ofisi za Makao Makuu jijini Dodoma.

Katika  maonesho hayo, Spika pia alizindua vitabu vitatu vya muongozo wa kusikiliza mashauri  mahakamani vinavyotumika  mahakama za mwanzo, mahakama za wilaya na mkoa na mahakama kuu.

Akizungumzia kuhusu vitabu hivyo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi, alisema vitabu vimeshawekwa kwenye tovuti ya Mahakama ya Tanzania.

Wiki ya hiyo imeanza Januari 31, mwaka huu na inatarajia kumalizika Februari 5 ambapo kilele chake cha siku ya sheria nchini kitafanyika Februari 6 jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius  Nyerere. Mgeni rasmi katika kilele hicho, anatarajiwa kuwa Rais wa Dk. John Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles