27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ndoo 60 za samaki wachanga zakamatwa Nyumba ya Mungu

Safina Sarwatt,Mwanga,

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limekamata ndoo 60 za samaki wachanga waliovuliwa kwa nyavu haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu  wakiwa wanafirishwa kwenda Arusha.

Samaki hao wamekamatwa leo Juni 18 majira saa tisa usiku katika kata ya Lag’ata wilayani Mwanga ambapo Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Hamis Issah, amewambia wandishi wa habari kuwa samaki hao walikamatwa wakiwa kwenye aina ya Mistubishi pajero yenye namba za usajili T. 527  AEQ na kwamba wanawashikilia watuhumiwa wawili walikutwa na samaki hao.

“Tumekata ndoo kubwa 60 za samaki wachanga ambao hawajafikia viwango na samaki hao wamevuliwa kwa kutumia kokoro hivyo jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wawili walikutwa na hawa samaki,” amesema.

Amewataja watuhumiwa hao ni mfanyabishara Godlisen Mfinanga (37), mkazi Mrombo Arusha na Mwidini Seleman (30) mkazi wa kisongo Arusha na kwamba watafikishwa Mahakamani.

Mkuu wa mkoa Kilimanjaro Dk. Anna Mghwira amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwasubua kwa zaidia ya miaka miwili, na kuipoteza halmashauri zaidi ya bilion 60 kutokana na uvuvi haramu unaendelea katika Bwawa ya nyumba ya Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles