28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nditiye akagua ufufuaji reli ya kaskazini

Na Mwandishi Wetu – Moshi

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara kukagua kazi ya ufufuaji wa reli kati ya Moshi hadi jijini Arusha kwa kutumia treni ya uhandisi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Lengo la ziara hiyo ni kuona maendeleo ya mradi wa ufuaji wa reli hiyo ambayo hivi karibuni itaanza kutoa huduma ya kusafirisha mizigo na abiria baada ya ufufuaji wake kukamilika kwa kiasi kikubwa. 

Sambamba na ukaguzi huo, shirika hilo hivi karibuni lilifanya ukaguzi wa kufanya tathmini ya ubora wa njia hiyo ya reli pamoja na kuendesha kampeni ya siku saba iliyoanza Agosti 3, mwaka huu ili kuongeza uelewa kwa wananchi wa Arusha, Moshi na Tanga kuhusu matumizi sahihi ya alama za usalama wa reli ili kuhakikisha reli na wananchi wanakuwa salama pindi treni zitakapoanza kutoa huduma.

Aliwataka wananchi wote wanaofanya shughuli za kijamii na kiuchumi, ikiwemo kilimo na biashara kandokando ya reli kuacha mara moja kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wao na miundombinu ya reli.

Alilitaka shirika kushirikiana kikamilifu na viongozi wa mikoa, wilaya na Serikali za mitaa kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu usalama wa reli na kuwa walinzi wa kwanza wa reli.

“Nimekagua njia iko vizuri, tunatarajia kuanza safari za treni kati ya Arusha na Moshi, baada ya wiki mbili au tatu kutoka sasa, shirika na viongozi wa mikoa hii wahakikishe wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu usalama wa reli,” alisema Nditiye.

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Reli, Focus Sahani alisema wataendelea kushirikiana na viongozi wa maeneo husika wakati wa kampeni ya uelewa ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa kuhusu usalama wa reli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles