26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

NDEMLA KUMFUATA ULIMWENGU WIKI IJAYO

NA JESSCA NANGAWE


DILI la kiungo mahiri wa Simba, Said Ndemla, kwenda kucheza soka la kulipwa Sweden limefikia hatua nzuri, ambapo anatarajia kusafiri nchini humo wiki ijayo.

Tayari klabu ya Simba imempa baraka zote kiungo huyo kwaajili ya kwenda kujaribu bahati yake katika klabu ya AFC Eskilistuna, inayomhitaji.

Akizungumza na MTANZANIA, meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu zitakazomruhusu mchezaji wake kuingia Sweden.

“Suala la Ndemla lipo kwenye hatua za mwisho, kinachosubiriwa ni hati yake ya kusafiria ambayo wakati wowote itatoka, tunaamini siku yoyote kuanzia Jumatatu anaweza kuondoka,” alisema Kisongo.

Ndemla alikuwa anahitajika katika klabu hiyo tangu  mwishoni mwa msimu uliopita, lakini uongozi wa Simba uliweka ngumu baada ya kudai bado ulikuwa unahitaji mchango wake katika kikosi cha Msimbazi.

Endapo kiungo huyo atafuzu majaribio yake, ataungana na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu, aliyejiunga na timu hiyo mapema Januari, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles