25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ndejembi amfunda Magufuli uenyekiti CCM

Pancras Ndejembi
Pancras Ndejembi

Na RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi, amemshauri Rais Dk. John Magufuli kuhakikisha anawapa nafasi vijana na wanawake pindi atakapokabidhiwa kijiti cha kuongoza chama Julai 23.

Amesema kundi la vijana na wanawake wamekuwa ni waaminifu katika nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Ndejembi ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga katika miaka ya 1980 hadi 2007, alisema kuwa mwenyekiti ajae wa CCM ambaye ni Rais Magufuli, aendelee kuwaamini vijana na wanawake kwa kuwateua katika nafasi mbalimbali kutokana na taaluma na utendaji wao, ili kujenga CCM mpya yenye matumaini mapya kwa Watanzania wote.

“Mwenyekiti mpya ajae katika chama chetu anatakiwa awape nafasi vijana pamoja na kina mama kwani wengi ni waadiliifu,’’ alisema.

Ndejembi aliwataka wanachama ambao wanajihisi wana harufu ya ufisadi ni vema waanze kukaa pembeni ili kuwaachia nafasi watu wengine wenye uwezo wa kuongoza.

“Ninawasihi wale wote wanaonyemelea kuchaguliwa wakati wanajihisi wananuka rushwa na wanaotumia mali za Watanzania kwa kujimilikisha, wafahamu kuwa awamu hii ya tano chini ya Dk. Magufuli kamwe wasitarajie kuchaguliwa, ni vizuri wakajiondoa,” alisema.

Pamoja na hayo, Ndejembi alitoa ushauri kwa vyama vya upinzani nchini kama vinataka kushika dola, ni lazima vijipange na kujiimarisha kwanza badala ya kufikiria kufanya fujo zisizokuwa na tija kwa taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles