26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Ndege yalipuka, 41 wafa Urusi

MOSCOW, URUSI

WATU 41 wamekufa baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Aeroflot kutua kwa dharura kabla ya kulipuka na kutekea moto kwenye Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo, Moscow.

Video katika mitandao ya jamii zinaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura kutoka kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikiteketea moto baada ya kutua vibaya.

Watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliokufa kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi.

Shahidi mmoja amesema ilikuwa ‘miujiza’ kuona kuna walionusurika katika mkasa wa ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 73 na wafanyakazi watano.

“Watu 37 wamenusurika ambao ni abiria 33 na wafanyakazi wanne,” alisema mmoja wa maofisa wa kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo, Yelena Markovskaya.

Aeroflot lilisema ndege hiyo ililazimika kurudi uwanjani kutokana na sababu za  ufundi  lakini halikufafanua.

Awali, ndege hiyo aina ya Sukhoi Superjet-100, iliondoka uwanja hapo saa 12:02 jioni kwa saa za hapa.

Marubani wakatoa tahadhari ya wasiwasi baada ya kushuhudia hitilafu muda mfupi baada ya ndege kuruka.

Baada ya kutua kwa dharura, huku sehemu za nyuma zikigusa ardhi, injini za ndege hiyo ziliwaka moto kwenye njia kuu ya ndege, Aeroflot lilisema katika taarifa.

Maofisa hao wa ndege “walijitahidi kadri ya uwezo wao kuwaokoa abiria,” waliofanikiwa kutolewa katika sekundi 55, shirika hilo la ndege limeeleza.

Taarifa pia zinaonyesha ndege hiyo haikufanikiwa katika jaribio la kwanza la kutua kwa dharura.

Kaimu Gavana wa mji eneo hilo la Murmansk, Andrey Chibis alisema familia za waliofariki duniua katika mkasa huo watalipwa dola 15,300 kila mmoja, huku waathirikwa watatibiwa katika hospitali na watapewa dola 7,650 kila mmoja.

Mmoja wa abiria, Mikhail Savchenko anasema alikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ikiwaka moto, lakini alifanikiwa kuruka nje.

Alituma video ya abiria waliokuwa wakihaha kutoka kwenye ndege na kuandika ujumbe: ‘niko sawa, niko hai na salama.’

Mmoja  wa manusura, Dmitry Khlebushkin, amesema anawashukuru wahudumu wa ndege hiyo kwa msaada wa hali na mali kuhakikisha wanatoka salama.

Uchunguzi umeidhinishwa sasa kufahamu zaidi kuhusu mkasa huo, taarifa zinasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles